Novemer 11 2012
TAARIFA YA HABARI YA USIKU
UMOJA HUO UMEISHUSHIA LAWAMA NZITO KAMPUNI HIYO YA KILIMANJARO MILLENIUM PRINTERS LTD(KPML) KWAMBA BAADHI YA WATUMISHI WAKE WAMEKUWA WAKIWATOZA ADHABU ZISIZOELEWAKA NA KUUTAKA UONGOZI WA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA KUINGILIA KATI SAKATA HILO.
AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA MADEREVA WENGINE ,MWENYEKITI WA UMOJA HUO,LOMAYANI MOLLEL ALISEMA KWAMBA BAADHI YA WATUMISHI WA KAMPUNI HIYO WAMEKUWA WAKIYAKATIA RISITI ZA MAEGESHO MAGARI YAO BILA TAARIFA YOYOTE KINYUME NA SHERIA.
HUKU AKIONYESHA KITABU CHA SHERIA NDOGO ZA USHURU WA KUEGESHA MAGARI CHA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA ,MOLLEL AMESEMA KWAMBA WAMEKUWA WAKITOZWA ADHABU MBALIMBALI KAMA KUEGESHA GARI BILA KULIPIA USHURU KIASI CHA SH,50,000,GHARAMA ZA KUPELEKA GARI KWENYE YADI SH,30,000 NA GHARAMA ZA KUTUNZA GARI HILO YADI SH,10,000 BADALA YA SH,50,000 ILIYOANISHWA KISHERIA.
WAPIGANAJI WA KUNDI
LA AL-SHABAB WAMEANZA KUEKELEA KATIKA ENEO LENYE MAMLAKA YA NDANI SOMALIA LA
PUNTLAND BAADA YA KUTIMULIWA NA VIKOSI VYA UMOJA WA AFRIKA KUSINI NA KATI MWA
NCHI HIYO PEMBE YA AFRIKA.
RAIS ABDIRAHMAN MOHAMUD FAROLE WA PUNTLAND AMEONYA KUWA WAPIGANAJI WA AL-SHABAB WANAWEZA KUIBUA MAPIGANO KATIKA ENEO HILO AMBALO LIMEKUWA LIKISHUHUDIA AMANI KINYUME MAENEO YA KUSINI NA KATI MWA SOMALIA.
AIDHA AMESEMA KUWA WAASI HAO WA AL-SHABAB HUENDA WAKAVURUGA SHUGHULI ZA UTAFUTAJI MAFUTA YA PETROLI KATIKA ENEO HILO.
KUFUATIA MAFANIKIO YA JESHI LA KENYA KATIKA KUWATIMUA WAASI WA AL SHABAB KATIKA NGOME YAO YA MWISHO MJINI KISMAYO, WAASI HAO SASA WANATAFUTA MAHALA PA KUKIMBILIA.
SERIKALI YA PUNTLAND IMEOMBA MSAADA WA KIMATAIFA KATIKA KUKABILIANA NA WAASI HAO WA AL-SHABAB.
LONDON:
MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA BBC, GEORGE ENTWISTLE, AMEJIUZULU.
MKURUGENZI HUYO AMEJIUZULU KUFUATIA KUSHUTUMIWA KWA NAMNA ALIVYOSHUGHULIKIA TAARIFA ILIYOPEPERUSHWA KATIKA KIPINDI CHA NEWSNIGHT.
TAARIFA HIYO KWA MAKOSA ILIMSHUTUMU ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA WAKATI WA SERIKALI YA CONSERVATIVE , LORD MCALPINE, KWAMBA ALIHUSIKA KATIKA KASHFA YA KUDHALILISHA WATOTO.
TAYARI SHIRIKA LA BBC LIMEKUWA LIKICHUNGUZWA VIKALI KATIKA KASHFA INAYOMHUSU MTANGAZAJI WAKE WA ZAMANI JIMMY SAVILE KWA MADAI YA KUWADHALILISHA WATOTO.
KIPINDI HICHO CHA NEWSNIGHT KINADAIWA KUACHA KWA MAKUSUDI KUTANGAZA HABARI YA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA KASHFA YA BWANA SAVILE.
NEWYORK:
UMOJA WA MATAIFA UMESEMA NIGERIA INAHITAJI MSAADA WA DHARURA WA DOLA MILIONI 38 KUWASAIDIA WATU MILIONI 2.1 WALIOPOTEZA MAKAO KUFUATIA MAFURIKO YA HIVI KARIBUNI NCHINI HUMO.
JENS LAERKE MSEMAJI WA OFISI YA UMOJA WA MATAIFA YA KURATIBU MISAADA YA KIBINAADAMU AMESEMA MISAADA INAYOHITAJIKA NI YA CHAKULA, MAJI SAFI, MAKAO YA MUDA NA SHULE KATIKA ENEO LA MTO NIGER.
MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA YAMESEMA MAFURIKO NCHINI NIGERIA YAMEATHIRI ZAIDI YA WATU MILIONI 7.7.
MAFURIKO HAYO AMBAYO YAMEELEZEWA KUWA MABAYA ZAIDI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 40, YAMESEMEKANA KUWAUA ZAIDI YA WATU MIA TATU, HUKU WENGINE ZAIDI YA MILIONI MBILI WAKIWA WAMEJIANDIKISHA KAMA WAKIMBIZI WA NDANI.
SHIRIKA LA AFYA DUNIANI, WHO LIMESEMA VISA VYA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA MALARIA VIMEONGEZEKA KUTOKANA NA MAFURIKO HAYO, INGAWA HAKUNA MLIPUKO MKUBWA ULIORIPOTIWA.
WHO PIA IMEELEZA UHARIBIFU ULIOFANYIKA DHIDI YA MAJENGO NA VIFAA VYA AFYA KATIKA MAENEO YALOATHIRIKA.
NALO SHIRIKA LA KUHUDUMIA WATOTO, UNICEF, LIMESEMA MAENEO YALOATHIRIKA HAYANA HUDUMA ZA MAJI SAFI, KWANI ASILIMIA 63 YA MAJI YA KUNYWA NA KUPIKIA HUTOKA KWENYE MITO NA VISIMA VILIVYO WAZI.
TAARIFA YA HABARI YA USIKU
MUSOMA
WITO UMETOLEWA KWA WENYEJI
WA MKOA WA MARA KUJIENDELEZA KIELIMU
ILI KUENDANA NA MABADILIKO YA SAYANSI
NA TEKNOLOJIA.
WITO HUO UMETOLEWA NA
KATIBU TAWALA MKOA WA MARA BWANA CLEMENT LUJAJI KAMA MGENI RASMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA, KATI KA MAHAFALI YA
WAHITIMU WA CHUO KIKUU HULIA TAWI LA MARA, YALIYO JANA SAMBAMBA NA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA
ISHIRINI TANGU KUANZISHWA HAPA NCHINI.
AKITOA TAARIFA FUPI YA
CHUO HICHO KWA MGENI RASMI, MKURUGENZI WA CHUO KIKUU TAWI
LA MKOA WA MARA BI, FLORA KIWONDE MESEMA JUMLA YA WAHITIMU 250 WAMEHITIMU
MASOMO YAO TANGU KUZINDULIWA KWA CHUO HICHO
MKOANI HUMO .
CHUO KIKUU HURIA TAWI LA
MARA KILIZINDULIWA RASMI 27-11-1999,AMBAPO KABLA YA HAPO WANACHUO WA CHUO KIKUU
HULIA WALIKUWA WANAPATA HUDUMA YA
MASOMO KATIKA CHUO KIKUU HULIA CHA MKOA WA MWANZA KATI YA 1994-1999.
AIDHA BI,KIWONDE AMETOA SHUKRANI KWA WADAU MBALIMBALI
WALIOJITOLEA KWA HALI NA MALI KUPATIKANA KWA MAFANIKIO YA CHUO KIKUU HURIA MKOA MARA NA KUSAIDIA CHUO KIKUU HULIA
TAWI LA MARA KUWA KATI YA VITUO BORA KITAIFA KWA MIAKA MIWILI MFULULIZO AMBAPO
MWAKA JUZI KILISHIKA NAFASI YA KWANZA KITAIFA NA MWAKA JANA KUSHIKA NAFASI YA
PILI KIKITANGULIWA NA MKOA WA ARUSHA.
DODOMA:
WAJUMBE
NA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI
WAMETAKIWA KUACHA TABIA YA KUTUMIA RUSHWA KWA LENGO LA
KUSHAWISHI KUCHAGULIWA AU KUTEULIWA KATIKA NYADHIFA MBALIMBALI ZA
UONGOZI .
HAYO
YAMESEMWA LEO NA MWENYEKITI WA TAIFA WA CHAMA CHA MAPINDUZI RAIS DR JAKAYA MRISHO KIKWETE KATIKA HOTUBA
YAKE ALIYOITOA MJINI DODOMA WAKATI AKIFUNGUA MKUTANO MKUU WA NANE WA CHAMA
HICHO ULIOANZA HII LEO NA AMBAO UTADUMU KWA SIKU MBILI.
AMESEMA
NI JAMBO LA FEDHEHA NA KUHUZUNISHA KWA
VIONGOZI AU BAADHI YA WAGOMBEA
KUTUMIA RUSHWA KATIKA KUSHAWISHI KUCHAGULIWA KATIKA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI ILI HALI WAKIJUA KWA KUFANYA
HIVYO NI KOSA KISHERIA .
KWA
UPANDE MWINGINE RAIS AMEWATAKA
WATANZANIA WANAOISHI KATIKA MIKOA YA MPAKA WA MALAWI NA TANZANIA KUISHI KWA AMANI NA UTULIVU NA KWAMBA
HAKUNA VITA YOYOTE ITAKAYOTOKEA KUTOKANA NA
MGOGORO HUO WA MPAKA WA MALAWI
NA TANZANIA NA KWAMBA HALI NI SHWARI .
AMESEMA TANZANIA HAINA MPANGO WA KUINGIA VITANI NA
MALAWI KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE NA
KWAMBA MAZUNGUMZO YATAENDELEA KAMA
KAWAIDA KUHAKIKISHA KUWA MGOGORO HUO
UNA MALIZWA KATIKA HALI YA MAZUNGUMZO .
ARUSHA:
UMOJA WA MADEREVA WA MAGARI MAKUBWA WALIOPO SOKO KUU JIJINI ARUSHA
WAMEISHUTUMU KAMPUNI ILIYOPEWA ZABUNI YA KUKUSANYA USHURU JIJINI HAPA KWAMBA
IMEKUWA IKIWANYANYASA KWA KUWATOZA ADHABU MBALIMBALI KINYEMELA SANJARI NA
KUKAMATA MAGARI YAO BILA SABABU ZA MSINGI.UMOJA HUO UMEISHUSHIA LAWAMA NZITO KAMPUNI HIYO YA KILIMANJARO MILLENIUM PRINTERS LTD(KPML) KWAMBA BAADHI YA WATUMISHI WAKE WAMEKUWA WAKIWATOZA ADHABU ZISIZOELEWAKA NA KUUTAKA UONGOZI WA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA KUINGILIA KATI SAKATA HILO.
AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA MADEREVA WENGINE ,MWENYEKITI WA UMOJA HUO,LOMAYANI MOLLEL ALISEMA KWAMBA BAADHI YA WATUMISHI WA KAMPUNI HIYO WAMEKUWA WAKIYAKATIA RISITI ZA MAEGESHO MAGARI YAO BILA TAARIFA YOYOTE KINYUME NA SHERIA.
HUKU AKIONYESHA KITABU CHA SHERIA NDOGO ZA USHURU WA KUEGESHA MAGARI CHA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA ,MOLLEL AMESEMA KWAMBA WAMEKUWA WAKITOZWA ADHABU MBALIMBALI KAMA KUEGESHA GARI BILA KULIPIA USHURU KIASI CHA SH,50,000,GHARAMA ZA KUPELEKA GARI KWENYE YADI SH,30,000 NA GHARAMA ZA KUTUNZA GARI HILO YADI SH,10,000 BADALA YA SH,50,000 ILIYOANISHWA KISHERIA.
ZANZIBAR:
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT ALI MOHAMED
SHEIN KESHO ANATARAJIWA KUFUNGUWA MKUTANO WA 34 WA JUIMUIA YA KIAFRIKA YA
UTUMISHI WA UMMA NA UONGOZI(AAPAM) HUKO ZANZIBAR BEACH RESORT NJE
KIDOGO WA MJI WA ZANZIBAR.
KWA
MUJIBU WA RATIBA ILIOTOLEWA NA JUMUIA HIYO IMEONESHA KUWA KATIBU WA
BARAZA LA MAPINDUZI NA KATIBU MKUU KIONGOZI DKT ABDULHAMID YAHYA MZEE ATATOWA
MAELEZO JUU YA MKUTANO HUO.
BAADAE RAIS WA AAPAM ABDON AGAW JOK NHIAL NAE ATATOWA MAELEZO JUU
YA MKUTANO HUO KWA UPANDE WA JUMUIA HIYO AMBAPO PIA WAZIRI WA NCHI
OFISI YA RAIS UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA WA SERIKALI YA JAMHURI YA
MUUNGANO TANZANIA CELINA KOMBANI ATATOWA MAELEZO NA BAADAE KUMKARIBISHA
MGENI RASMI RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT ALI
MOHAMED SHEIN AMBAE ATAHUTUBIA MKUTANO HUO.
WAJUMBE KADHAA WA MKUTANO HUO TAYARI WAMESHAWASILI ZANZIBAR
AKIWAMO KATIBU MKUU WA AAPAM .
JUMLA YA WAJUMBE 500 WANATARAJIWA KUSHIRIKI KATIKA MKUTANO HUO
AMBAPO MWAKA JANA MKUTANO KAMA HUO ULIFANYIKA NCHINI MALAWI.
MBALI NA MKUTANO HUO WAJUMBE HAO PIA WATAPATA FURSA YAKUTEMBELEA SEHEMU
MBALIMBALI ZA VIVUTIO VYA UTALII VILIOPO ZANZIBAR PAMOJA NA KUTEMBELEA
MJI MKONGE NA SEHEMU ZA HISTORIA.
MKUTANO HUO WA AAPAM WA SIKU TANO UNATARAJIWA KUMALIZIKA TAREHE
16/11/2012
UNAENDELEA KUSIKILIZA TAARIFA YA HABARI KUTOKA VICTORIA FM,
ZIFUATAZO SASA NI HABARI ZA KIMATAIFA.
KAMPALA :
WAZIRI WA
ULINZI WA UGANDA CRISPUS KYONGA AMESEMA SERIKALI YA UGANDA IMEWAHI KUFANYA
MAZUNGUMZO NA WAKUU WA M23 INGAWA MAZUNGUMZO HAYO YALIPATA BARAKA KUTOKA KWA
RAIS JOSEPH KABILA WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO.
KYONGA
AMESEMA MAZUNGUMZO HAYO YALIYOFANYIKA KAMPALA YALIKUWA NA LENGO LA KUANDAA
MAZINGIRA YA KUFANYIKA MAZUNGUMZO KATI YA WAASI HAO NA SERIKALI YA KINSHASA.
MWISHONI MWA
MWEZI ULIOPITA, UMOJA WA MATAIFA ULITOA RIPOTI INAYODAI KWAMBA UGANDA NA RWANDA
ZIMEKUWA ZIKIWAUNGA MKONO WAASI HAO WA DRC. KUFUATIA RIPOTI HIYO, UGANDA
ILITISHIA KUWAONDOA WANAJESHI WAKE WANAOSHIRIKI JUHUDI ZA KULINDA AMANI KATIKA
NCHI MBALIMBALI ZA DUNIA HUSUSAN SOMALIA.
TAYARI UMOJA
WA MATAIFA UMESEMA RIPOTI HIYO INAAKISI MISIMAMO BINAFRSI YA WATAALAMU WA
BARAZA LA USALAMA NA WALA SIO UMOJA WA MATAIFA KWA UJUMLA.
PUNTLAND: