Wednesday, January 9, 2013

MWANDISHI WA RADIO KWIZERA ISSA NGUMBA AKUTWA AMEUAWA PORINI

                                                      Marehemu Issa Ngumba
   MWANDISHI wa Habari wa kituo cha Radio Kwizera wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Issa        Ngumba (45) ameua kwa kunyongwa na kisha kupigwa risasi mkono wa kushoto huku simu zake mbili na Bastola iliyotumika kumshambulia ikiacha kando ya mwili wake porini.

Habari zilizopenyezwa kutoka wilayani Kakonko mkoani Kigoma na kuthibitishwa na kamanda wa Polisi wa mkoa huo Frasser Kashai, pamoja na Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Kigoma (KPC) Deo Sonkolo zimedai kuwa mwandishi huyo amekutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na watu ambao hawajajulikana.

Akizungumza na kwa njia ya simu, Sonkolo alisema kwamba mara baada ya kupata taarifa hizo aliwasiliana na waandishi habari wilaya ya Kibondo ambao waliwahi kufika eneo la tukio na kushuhudia uchunguzi wa Daktari Primus. Mwili wa marehemu umepatikana leo katika pori la Mlima Kajuluheta kijiji cha Muhange, wilayani humo majira ya asubuhi baada ya wananchi kufanya msako wa siku tatu tokea siku ua Jumapili ikiwa ni siku moja baada ya kutoonekana kwake.

Bastola iliyokutwa eneo la tukio imeokotwa ikiwa na risasi tano huku mifuko ya suruali ya marehemu ikiwa na noti moja ya Tsh10,000.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Frasser Kashai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa jeshi lake bado linangoja taarifa ya uchunguzi wa daktari sanjari na taarifa ya awali ya uchunguzi wa jeshi hilo toka eneo la tukio.

1 comment:

  1. Merkur 37C Safety Razor Review – Merkur 37C
    The Merkur 37c is 바카라 사이트 an excellent https://deccasino.com/review/merit-casino/ short https://deccasino.com/review/merit-casino/ handled DE safety razor. It is more suitable kadangpintar for both heavy and non-slip ventureberg.com/ hands and is therefore a great option for experienced

    ReplyDelete