NEWS


Novemer 11 2012 

                    TAARIFA YA HABARI YA USIKU


 MUSOMA

WITO UMETOLEWA KWA WENYEJI WA MKOA WA MARA  KUJIENDELEZA KIELIMU ILI KUENDANA  NA MABADILIKO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

WITO HUO UMETOLEWA NA KATIBU TAWALA MKOA WA MARA BWANA CLEMENT LUJAJI  KAMA MGENI RASMI KWA NIABA YA MKUU WA  MKOA, KATI KA  MAHAFALI YA WAHITIMU WA CHUO KIKUU HULIA TAWI LA MARA, YALIYO JANA  SAMBAMBA NA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA ISHIRINI TANGU KUANZISHWA HAPA NCHINI.

AKITOA TAARIFA FUPI YA CHUO  HICHO KWA  MGENI RASMI, MKURUGENZI WA CHUO KIKUU TAWI LA MKOA WA MARA BI, FLORA KIWONDE MESEMA JUMLA YA WAHITIMU 250 WAMEHITIMU MASOMO YAO TANGU KUZINDULIWA KWA CHUO HICHO  MKOANI HUMO .

CHUO KIKUU HURIA TAWI LA MARA KILIZINDULIWA RASMI 27-11-1999,AMBAPO KABLA YA HAPO WANACHUO WA CHUO KIKUU HULIA WALIKUWA WANAPATA  HUDUMA YA MASOMO KATIKA CHUO KIKUU HULIA CHA MKOA WA MWANZA KATI YA 1994-1999. 

AIDHA BI,KIWONDE  AMETOA SHUKRANI KWA WADAU MBALIMBALI WALIOJITOLEA KWA HALI NA MALI KUPATIKANA KWA MAFANIKIO YA CHUO KIKUU  HURIA MKOA MARA NA KUSAIDIA CHUO KIKUU HULIA TAWI LA MARA KUWA KATI YA VITUO BORA KITAIFA KWA MIAKA MIWILI MFULULIZO AMBAPO MWAKA JUZI KILISHIKA NAFASI YA KWANZA KITAIFA NA MWAKA JANA KUSHIKA NAFASI YA PILI KIKITANGULIWA NA MKOA WA ARUSHA.
 

DODOMA:

WAJUMBE NA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI  WAMETAKIWA  KUACHA TABIA YA  KUTUMIA RUSHWA  KWA LENGO LA  KUSHAWISHI  KUCHAGULIWA  AU KUTEULIWA KATIKA NYADHIFA MBALIMBALI ZA UONGOZI .

HAYO YAMESEMWA LEO NA MWENYEKITI WA TAIFA WA CHAMA CHA MAPINDUZI  RAIS DR JAKAYA MRISHO KIKWETE KATIKA HOTUBA YAKE ALIYOITOA MJINI DODOMA WAKATI AKIFUNGUA MKUTANO MKUU WA NANE WA CHAMA HICHO  ULIOANZA HII LEO   NA AMBAO UTADUMU KWA SIKU MBILI.

AMESEMA NI JAMBO LA FEDHEHA NA KUHUZUNISHA   KWA VIONGOZI  AU BAADHI YA   WAGOMBEA  KUTUMIA RUSHWA KATIKA KUSHAWISHI KUCHAGULIWA  KATIKA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI ILI HALI WAKIJUA KWA KUFANYA HIVYO  NI KOSA KISHERIA .

KWA UPANDE MWINGINE RAIS   AMEWATAKA WATANZANIA WANAOISHI KATIKA MIKOA YA MPAKA WA MALAWI NA TANZANIA   KUISHI KWA AMANI NA UTULIVU NA KWAMBA HAKUNA VITA YOYOTE ITAKAYOTOKEA KUTOKANA NA   MGOGORO HUO WA MPAKA   WA MALAWI NA TANZANIA  NA KWAMBA HALI NI SHWARI .

AMESEMA  TANZANIA HAINA MPANGO WA KUINGIA VITANI NA MALAWI KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE  NA KWAMBA MAZUNGUMZO YATAENDELEA  KAMA KAWAIDA KUHAKIKISHA KUWA   MGOGORO HUO UNA MALIZWA KATIKA HALI YA MAZUNGUMZO .


ARUSHA:
UMOJA WA MADEREVA WA MAGARI MAKUBWA WALIOPO SOKO KUU JIJINI ARUSHA WAMEISHUTUMU KAMPUNI ILIYOPEWA ZABUNI YA KUKUSANYA USHURU JIJINI HAPA KWAMBA IMEKUWA IKIWANYANYASA KWA KUWATOZA ADHABU MBALIMBALI KINYEMELA SANJARI NA KUKAMATA MAGARI YAO BILA SABABU ZA MSINGI.
UMOJA HUO UMEISHUSHIA LAWAMA NZITO KAMPUNI HIYO YA KILIMANJARO MILLENIUM PRINTERS LTD(KPML) KWAMBA BAADHI YA WATUMISHI WAKE WAMEKUWA WAKIWATOZA ADHABU ZISIZOELEWAKA NA KUUTAKA UONGOZI WA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA KUINGILIA KATI SAKATA HILO.
AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA MADEREVA WENGINE ,MWENYEKITI WA UMOJA HUO,LOMAYANI MOLLEL ALISEMA KWAMBA BAADHI YA WATUMISHI WA KAMPUNI HIYO WAMEKUWA WAKIYAKATIA RISITI ZA MAEGESHO MAGARI YAO BILA TAARIFA YOYOTE KINYUME NA SHERIA.
HUKU AKIONYESHA KITABU CHA SHERIA NDOGO ZA USHURU WA KUEGESHA MAGARI CHA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA ,MOLLEL AMESEMA KWAMBA WAMEKUWA WAKITOZWA ADHABU MBALIMBALI KAMA KUEGESHA GARI BILA KULIPIA USHURU KIASI CHA SH,50,000,GHARAMA ZA KUPELEKA GARI KWENYE YADI SH,30,000 NA GHARAMA ZA KUTUNZA GARI HILO YADI SH,10,000 BADALA YA SH,50,000 ILIYOANISHWA KISHERIA.

ZANZIBAR:

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT ALI MOHAMED SHEIN KESHO ANATARAJIWA KUFUNGUWA MKUTANO WA 34 WA JUIMUIA YA KIAFRIKA YA UTUMISHI WA UMMA  NA UONGOZI(AAPAM) HUKO ZANZIBAR BEACH RESORT NJE KIDOGO WA MJI WA ZANZIBAR.
 KWA MUJIBU WA RATIBA ILIOTOLEWA NA JUMUIA HIYO IMEONESHA KUWA KATIBU  WA BARAZA LA MAPINDUZI NA KATIBU MKUU KIONGOZI DKT ABDULHAMID YAHYA MZEE ATATOWA MAELEZO JUU YA MKUTANO HUO.

BAADAE RAIS WA AAPAM ABDON AGAW JOK NHIAL NAE ATATOWA MAELEZO JUU  YA MKUTANO HUO  KWA UPANDE WA JUMUIA HIYO AMBAPO PIA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA WA SERIKALI YA JAMHURI  YA MUUNGANO TANZANIA  CELINA KOMBANI ATATOWA MAELEZO NA BAADAE KUMKARIBISHA MGENI RASMI RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT ALI MOHAMED SHEIN AMBAE ATAHUTUBIA MKUTANO HUO.

WAJUMBE KADHAA WA MKUTANO HUO TAYARI WAMESHAWASILI ZANZIBAR  AKIWAMO KATIBU MKUU WA AAPAM .

JUMLA  YA WAJUMBE 500 WANATARAJIWA KUSHIRIKI KATIKA MKUTANO HUO AMBAPO MWAKA JANA  MKUTANO  KAMA HUO ULIFANYIKA NCHINI MALAWI.

MBALI NA MKUTANO HUO WAJUMBE HAO PIA WATAPATA FURSA YAKUTEMBELEA SEHEMU MBALIMBALI ZA VIVUTIO VYA UTALII  VILIOPO ZANZIBAR PAMOJA NA KUTEMBELEA MJI MKONGE NA SEHEMU ZA HISTORIA.

MKUTANO HUO WA AAPAM WA SIKU TANO UNATARAJIWA KUMALIZIKA TAREHE 16/11/2012


UNAENDELEA KUSIKILIZA TAARIFA YA HABARI KUTOKA VICTORIA FM, ZIFUATAZO SASA NI HABARI ZA KIMATAIFA.

KAMPALA :

WAZIRI WA ULINZI WA UGANDA CRISPUS KYONGA AMESEMA SERIKALI YA UGANDA IMEWAHI KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAKUU WA M23 INGAWA MAZUNGUMZO HAYO YALIPATA BARAKA KUTOKA KWA RAIS JOSEPH KABILA WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO.

KYONGA AMESEMA MAZUNGUMZO HAYO YALIYOFANYIKA KAMPALA YALIKUWA NA LENGO LA KUANDAA MAZINGIRA YA KUFANYIKA MAZUNGUMZO KATI YA WAASI HAO NA SERIKALI YA KINSHASA.

MWISHONI MWA MWEZI ULIOPITA, UMOJA WA MATAIFA ULITOA RIPOTI INAYODAI KWAMBA UGANDA NA RWANDA ZIMEKUWA ZIKIWAUNGA MKONO WAASI HAO WA DRC. KUFUATIA RIPOTI HIYO, UGANDA ILITISHIA KUWAONDOA WANAJESHI WAKE WANAOSHIRIKI JUHUDI ZA KULINDA AMANI KATIKA NCHI MBALIMBALI ZA DUNIA HUSUSAN SOMALIA.

TAYARI UMOJA WA MATAIFA UMESEMA RIPOTI HIYO INAAKISI MISIMAMO BINAFRSI YA WATAALAMU WA BARAZA LA USALAMA NA WALA SIO UMOJA WA MATAIFA KWA UJUMLA.

PUNTLAND:

WAPIGANAJI WA KUNDI LA AL-SHABAB WAMEANZA KUEKELEA KATIKA ENEO LENYE MAMLAKA YA NDANI SOMALIA LA PUNTLAND BAADA YA KUTIMULIWA NA VIKOSI VYA UMOJA WA AFRIKA KUSINI NA KATI MWA NCHI HIYO PEMBE YA AFRIKA.
RAIS ABDIRAHMAN MOHAMUD FAROLE WA PUNTLAND AMEONYA KUWA WAPIGANAJI WA AL-SHABAB WANAWEZA KUIBUA MAPIGANO KATIKA ENEO HILO AMBALO LIMEKUWA LIKISHUHUDIA AMANI KINYUME MAENEO YA KUSINI NA KATI MWA SOMALIA.
AIDHA AMESEMA KUWA WAASI HAO WA AL-SHABAB HUENDA WAKAVURUGA SHUGHULI ZA UTAFUTAJI MAFUTA YA PETROLI KATIKA ENEO HILO.
KUFUATIA MAFANIKIO YA JESHI LA KENYA KATIKA KUWATIMUA WAASI WA AL SHABAB KATIKA NGOME YAO YA MWISHO MJINI KISMAYO, WAASI HAO SASA WANATAFUTA MAHALA PA KUKIMBILIA.
SERIKALI YA PUNTLAND IMEOMBA MSAADA WA KIMATAIFA KATIKA KUKABILIANA NA WAASI HAO WA AL-SHABAB.

LONDON:
MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA BBC, GEORGE ENTWISTLE, AMEJIUZULU.
MKURUGENZI HUYO AMEJIUZULU KUFUATIA  KUSHUTUMIWA KWA NAMNA ALIVYOSHUGHULIKIA TAARIFA ILIYOPEPERUSHWA KATIKA KIPINDI CHA NEWSNIGHT.
TAARIFA HIYO KWA MAKOSA ILIMSHUTUMU ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA WAKATI WA SERIKALI YA CONSERVATIVE , LORD MCALPINE, KWAMBA ALIHUSIKA KATIKA KASHFA YA KUDHALILISHA WATOTO.
TAYARI SHIRIKA LA BBC LIMEKUWA LIKICHUNGUZWA VIKALI KATIKA KASHFA INAYOMHUSU MTANGAZAJI WAKE WA ZAMANI JIMMY SAVILE KWA MADAI YA KUWADHALILISHA WATOTO.
KIPINDI HICHO CHA NEWSNIGHT KINADAIWA KUACHA KWA MAKUSUDI KUTANGAZA HABARI YA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA KASHFA YA BWANA SAVILE.

NEWYORK:

UMOJA WA MATAIFA UMESEMA NIGERIA INAHITAJI MSAADA WA  DHARURA WA DOLA MILIONI 38 KUWASAIDIA WATU MILIONI 2.1 WALIOPOTEZA MAKAO KUFUATIA MAFURIKO YA HIVI KARIBUNI NCHINI HUMO.
JENS LAERKE MSEMAJI WA OFISI YA UMOJA WA MATAIFA YA KURATIBU MISAADA YA KIBINAADAMU AMESEMA MISAADA INAYOHITAJIKA NI YA CHAKULA, MAJI SAFI, MAKAO YA MUDA NA SHULE KATIKA ENEO LA MTO NIGER.
MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA YAMESEMA MAFURIKO NCHINI NIGERIA YAMEATHIRI ZAIDI YA WATU MILIONI 7.7.
MAFURIKO HAYO AMBAYO YAMEELEZEWA KUWA MABAYA ZAIDI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 40, YAMESEMEKANA KUWAUA ZAIDI YA WATU MIA TATU, HUKU WENGINE ZAIDI YA MILIONI MBILI WAKIWA WAMEJIANDIKISHA KAMA WAKIMBIZI WA NDANI.
SHIRIKA LA AFYA DUNIANI, WHO LIMESEMA VISA VYA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA MALARIA VIMEONGEZEKA KUTOKANA NA MAFURIKO HAYO, INGAWA HAKUNA MLIPUKO MKUBWA ULIORIPOTIWA.
WHO PIA IMEELEZA UHARIBIFU ULIOFANYIKA DHIDI YA MAJENGO NA VIFAA VYA AFYA KATIKA MAENEO YALOATHIRIKA.
NALO SHIRIKA LA KUHUDUMIA WATOTO, UNICEF, LIMESEMA MAENEO YALOATHIRIKA HAYANA HUDUMA ZA MAJI SAFI, KWANI ASILIMIA 63 YA MAJI YA KUNYWA NA KUPIKIA HUTOKA KWENYE MITO NA VISIMA VILIVYO WAZI.