SPORTS

KATIKA ZIGZAGA LA KIMICHEZO HII LEO NDANI YA VICTORIA FM

            NA MWANANDINGA WAKO MACK JUMANNE  

Hizi ni habari ambazo zimejili kwa juma zima hapa victoria fm ni kila siku ya jumapili kuanzia 10 kamili hadi 11 kamili


 

BPL: LEO ndio LEO kwa Chelsea, Liverpool, City na Spurs!!

CHELSEACITY KUWASOGELEA VINARA MAN UNITED??

RATIBA:
Jumapili, Novemba 11
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Manchester City v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Newcastle United v West Ham United
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Liverpool
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Leo, kwenye mfululizo wa Mechi za Ligi Kuu England, BPL, zipo Mechi 3 lakini mbili ndio zipo kwenye midomo ya Wadau wengi wa Soka, zile za Manchester City v Tottenham Hotspur na Chelsea v Liverpool, hasa kwa vile zinahusisha Timu vigogo na pia kutaka kujua kama Chelsea na City wanaweza kuikaribia Manchester United ambao ndio vinara na jana walipiga hatua zaidi mbele baada ya kuibonda Aston Villa 3-2 na kuwafanya waongoze Ligi wakiwa Pointi 4 mbele ya Chelsea walio nafasi ya pili na Pointi 5 mbele ya City walio nafasi ya 3.
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man United Mechi 11 Pointi 27
2 Chelsea Mechi 10 Pointi 23
3 Man City  Mechi 10 Pointi 22

Manchester City v Tottenham
Manchester City wataingia kwenye Mechi hii wakitegemea kuwa nao tena Joleon Lescott, Maicon na David Silvaambao walikuwa majeruhi lakini Wachezaji Micah Richards, James Milner na Jack Rodwell kwa vile bado ni majeruhi.
Tottenham itakuwa bila majeruhi Mousa Dembele, Scott Parker, Benoit Assou-Ekotto na Younes Kaboul.

VIKOSI VINATARAJIWA:

Manchester City: Hart, Pantilimon, Wright, Zabaleta, Maicon, Kompany, Lescott, Nastasic, K Toure, Clichy, Kolarov, Nasri, Y Toure, Barry, Garcia, Sinclair, Silva, Aguero, Dzeko, Balotelli, Tevez.
Tottenham: Friedel, Lloris, Cudicini, Gomes, Naughton, Walker, Caulker, Gallas, Dawson, Vertonghen, Livermore, Parrett, Huddlestone, Mason, Carroll, Sandro, Sigurdsson, Lennon, Townsend, Bale, Falque, Dempsey, Obika, Defoe, Adebayor.
Newcastle v West Ham
Newcastle watacheza bila ya Cheick Tiote na Fabricio Coloccini ambao wapo kifungoni.
Meneja wa West Ham Sam Allardyce yupo kwenye hali tete kwani hana uhakika wa Mabeki wake James Collins na James Tomkins kuwepo kwa vile wana maumivu.

VIKOSI VINATARAJIWA:

Newcastle: Krul, Harper, Elliot, Santon, Ferguson, Tavernier, S. Taylor, Williamson, Bigirimana, Cabaye, Gutierrez, Ben Arfa, Anita, Obertan, Sammy Ameobi, Marveaux, Amalfitano, Abeid, Ba, Cisse, Shola Ameobi, Xisco.
West Ham: Jaaskelainen, Spiegel, O'Brien, Reid, Collins, Tomkins, McCartney, Demel, Noble, Diame, Nolan, Jarvis, Benayoun, Diarra, O'Neil, Maiga, Cole, Carroll, Spence.

Chelsea v Liverpool

Ashley Cole hatakuwepo kwenye Kikosi cha Chelsea kwa vile ni majeruhi lakini John Terry anaweza kuanza baada ya kumaliza Kifungo chake cha Mechi 4 kwa Ubaguzi.
Beki wa England Glen Johnson anatarajiwa kurudi dimbani baada ya kupona maumivu ya musuli za pajani na pia Kipa Jose Reina huenda akawemo baada ya pia kupona.

VIKOSI VINATARAJIWA:

Chelsea: Cech, Ivanovic, Azpilicueta, Terry, Luiz, Cahill, Bertrand, Mikel, Romeu, Ramires, Mata, Oscar, Hazard, Moses, Marin, Torres, Sturridge, Turnbull
Liverpool: Jones, Gulacsi, Reina, Wisdom, Agger, Skrtel, Coates, Carragher, Enrique, Johnson, Downing, Allen, Sahin, Gerrard, Shelvey, Henderson, Assaidi, Yesil, Suso, Suarez, Sterling
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

 HAPA NYUMBANI

VPL: SIMBA AZAM ZACHAPWA, YANGABADO JUU!

Bao la Dakika ya 73 la Musa Saidi Kimbu, limeipa ushindi ‘Wapwa’ wa Yanga, Toto African, wa bao 1-0 dhidi ya Simba katika Mechi ya Ligi Kuu Vodacom, VPL,  iliyochezwa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na huko Tanga Mgambo JKT imewachapa Azam FC bao 2-1 na matokeo haya yamewabakisha Yanga kileleni na kesho wana nafasi ya kuzidisha pengo la uongozi wao watakapocheza huko Mkwakwani, Tanga na Coastal Union.


MSIMAMO TIMU ZA JUU 
Msimamo huu utazingatia matokeo ya leo ambapo yanga iko dimbani na wagosi wa kaya costal union

1 Yanga Mechi 12 Pointi 26
2 Azam FC Mechi 13 Pointi 24
3 Simba Mechi 13 Pointi 23
4 Coastal Mechi 12 Pointi 22
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Simba walicheza Mechi ya leo bila Kipa wao Nambari Wani Juma Kaseja ambae amepumzika baada ya kuletewa kashikashi na Mashabiki wa Simba walipofungwa na Mtibwa Sugar bao 2-0 katika Mechi yao iliyopita huko Manungu, Morogoro.
Huko Tanga, Mgambo JKT nao wameshusha balaa kwa Azam FC kwa kuwashushia kipigo cga bao 2-1 ambacho kimewakosesha kutwaa uongozi wa Ligi.
Jumapili, Novemba 11, Yanga, ambao ndio vinara wa Ligi  kwa Pointi 2 mbele ya Azam, watakuwa huko Mkwakwani, Tanga kucheza na Coastal Union na wakishinda watafungua pengo la Pointi 5 mbele.

RATIBA/MATOKEO:

Mgambo JKT 2 Azam 1
African Lyon v Mtibwa Sugar [Azam Complex, Dar es Salaam]
Simba 0 Toto Africans 1
Tanzania Prisons v JKT Ruvu [Sokoine, Mbeya]
Kagera Sugar v Polisi Morogoro [Kaitaba, Kagera]
JKT Oljoro v Ruvu Shootings [Sheikh Amri Abeid, Arusha]
Jumapili Novemba 11
Coastal Union v Yanga [Mkwakwani, Tanga]
 ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,